UONGOZI WA JUU WA CHADEMA UNAHUSIKA MOJA KWA MOJA NA UTEUZI WA WABUNGE WA VITI MAALUM WALIO APA TAREHE 24/11/2020
Tarehe 25/11/2020 Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika aliongea na waandishi wa habari mambo mengi yakujibaraguza kuhusu wabunge wa viti maalum walioapishwa siku ya tarehe 24.11.2020 na Mhe. Spika Job Ndugai Jijini Dodoma. Kama ulipata bahati ya kumsikiliza Mnyika vizuri basi utaelewa kuwa CHADEMA wanawachezea mchezo wa mind-game wafuasi wao kuwa hawahusiki na tukio hilo la kuteua wabunge hao wakati hali halisi ni kuwa wanahusika kwa asilimia zote. Mambo haya ni uthibitisho kuwa CHADEMA inahusika moja kwa moja na uteuzi wa wabunge hao:- 1. Kamati kuu ya CHADEMA ingekutana kwa dharura tangu jana (hata kwa kufanya online meeting kama walivyowai kufanya kipindi kile walivyokimbia vikao vya bungeni kwa kudai kuwa wanajilinda na COVID-19) na leo wangekuja na jibu la moja kwa moja kuhusu wabunge hao kwasababu ni tukio kubwa mno ndani ya chama hicho. 2. Tutaaminije kama tukio hilo halina Baraka kutoka uongozi wa juu wa chama, makaratasi aliyoyaonesha Mnyika eti hajayajaza what if ni cop