WALICHOSEMA TEC NI USHAURI KAMA WALIVYOFANYA MWAKA 2020. TUSIPOTOSHE
Vyombo vya ndani na nje vimekuwa mstari wa mbele kupotosha waraka uliotolewa na Baraza la Maaskofu Tanzania ( TEC) kuhusu kujilinda na virusi vipya vinavyosababisha virusi vya corona vilivyogunduliwa Afrika ya Kusini na Uingereza. Wakati Baraza la Maaskofu likiwaomba watanzania kuchukua tahadhali kwa kuwa Tanzania sio kisiwa, vyombo vya habari vimesema Baraza limesema Tanzania kuna virusi hivyo vipya. Ukweli ni kwamba ukisoma waraka huo hauna tofauti kubwa na ule walioutoa mwaka 2020 mwezi wa pili ukiwaomba watanzania kuchukua tahadhali. Ikumbukwe kuwa dini na viongozi wote wa imani wanalo jukumu la kuwakumbusha waumini kutenda na kuishi maisha mema. Hili ndo walilofanya Baraza la Maaskofu kuwakumbusha waamini wao na watanzania kwa ujumla kutokubweteka na kuendelea kufuata miongozo iliyotolewa na wizara ya afya ya kunawa mikono, kuvaa barakoa, kuepuka misongamano isiyo ya lazima na mingine mingi. Ni kwa msingi huo ukisoma waraka huo hakuna popote unaposema Tanzania kuna virusi vipya vi