Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti, 2020

DAVID KAFULILA APANGUA HOJA 7 ZA TUNDU LISSU KWA TAKWIMU

Picha
Na David KAFULILA, Agosti 31, 2020. Kwanza nashukuru sasa kuona ndugu yangu Tundu Lissu ameanza kuleta hoja zinazoweza kuanza kujadilika kama mgombea, tofauti na mwanzo ambapo ilikuwa ni masimulizi ambayo kwakweli hayakuwa na lolote la kusaidia maamuzi ya mpiga kura. Jana nilifuatilia hotuba yake iliyokosoa masuala kadhaa ambayo nimeona si busara ayatumie kupotosha Watanzania kufanya maamuzi katika misingi ya upotoshaji. Ili kurahisisha, nimepanga mawazo yangu katika mafungu 7; 1. Lissu anasema Ripoti ya Benki ya Dunia ya Mwaka huu 2020 kuhusu urahisi wa kufanya Biashara( Easy of Doing Business Report 2020) imeishusha Tanzania kutokana na utawala wa JPM. Asichokijua Lissu na wenzake wanaotumia hoja hiyo ni kwamba tayari Benki hiyo hiyo ya dunia (WB), katika taarifa yake ya tarehe ya juzi Agosti 27,2020, imeifuta tathimini hiyo ya Mwaka 2020 na ile ya 2018.  Benki ya Dunia imeleza wazi kuwa tathimini hizo zilikuwa na kasoro nyingi za kiuweledi na hivyo kukosa uhalisia. Kwa maelezo zaidi