Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Desemba, 2020

Aliyegombea Ubunge Jimbo la Siha kupitia Chadema Elvis Christopher Mosi Atimukia CCM

Picha
Wakati Tukielekea Kuupokea Mwaka 2021 Leo Aliyekuwa Mgombea Ubunge Jimbo la Siha Kwa Tiketi Ya Chadema Kamanda ELVIS CHRISTOPHER MOSI Leo Amemwaga Manyanga na Kujiunga Na Chama Cha Mapinduzi. Aidha, Ndugu ELVIS CHRISTOPHER MOSI  Ameamua Kujiunga na Chama Cha Mapinduzi Kutokana na Sera za Chama Cha Mapinduzi Zilizojikita Katika Kuleta Maendeleo Kwa WaTanzania. Sambamba na Zoezi Hilo Pia Aliyekuwa Katibu Wa Chadema Wilaya ya Siha na Mjumbe wa Baraza Kuu Chadema Taifa Kamanda Emanuel Nabora Amestaafu Siasa na Kuachana Na Nafasi Zake Zote Ndani Ya Chadema.

Rais Dkt.John Pombe Magufuli akagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kigongo-Busisi la Mkoani Mwanza

Picha
RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli aliwataka Watanzania kuzitumia mvua zinazoendelea kunyesha  kulima mazao ya biashara ili kuweza kuziuzia nchi zinazokabiliwa na janga la Corona, huku akimtaka mkandarasi wa daraja la Kigongo Busisi kumaliza kazi hiyo ndani ya miaka mitatu na siyo miaka minne. Rais Magufuli aliyasema hayo leo Jumatatu, Desemba 28, 2020 wakati alipofanya ziara ya kushitukiza katika daraja hilo linalotarajia kukamilika kwa gharama ya bilioni 700. “Watanzania tunatakiwa kumshukuru Mungu kwa kutuepusha na janga la Corona na tulime kwa nguvu zote ili kukuza uchumi wa nchi na watu kwa ujumla,mazao mtakayolima tutaziuzia nchi zinazokabiliwa na Corona maana watu wao hawafanyi kazi wapo kwenye karantini,” alisema Magufuli. Alisema wananchi walime sana maana mwakani nchi inaweza kukabiliwa na janga la njaa,kutokana na nchi nyingi zitahitaji chakula kutoka Tanzania. Aidha, Magufuli alimtaka mkandarasi anayejenga daraja la Kigogo Busisi wa