Rais Dkt.John Pombe Magufuli akagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kigongo-Busisi la Mkoani Mwanza
RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli aliwataka Watanzania kuzitumia mvua zinazoendelea kunyesha kulima mazao ya biashara ili kuweza kuziuzia nchi zinazokabiliwa na janga la Corona, huku akimtaka mkandarasi wa daraja la Kigongo Busisi kumaliza kazi hiyo ndani ya miaka mitatu na siyo miaka minne.
Rais Magufuli aliyasema hayo leo Jumatatu, Desemba 28, 2020 wakati alipofanya ziara ya kushitukiza katika daraja hilo linalotarajia kukamilika kwa gharama ya bilioni 700. “Watanzania tunatakiwa kumshukuru Mungu kwa kutuepusha na janga la Corona na tulime kwa nguvu zote ili kukuza uchumi wa nchi na watu kwa ujumla,mazao mtakayolima tutaziuzia nchi zinazokabiliwa na Corona maana watu wao hawafanyi kazi wapo kwenye karantini,” alisema Magufuli.
Alisema wananchi walime sana maana mwakani nchi inaweza kukabiliwa na janga la njaa,kutokana na nchi nyingi zitahitaji chakula kutoka Tanzania. Aidha, Magufuli alimtaka mkandarasi anayejenga daraja la Kigogo Busisi wa Kampuni ya China Civil Engineering Group Limited kwa gharama ya Tsh. bilioni 700, kujenga miradi huo usiku na mchana ili kukamilisha ndani ya miaka mitatu, maana ilitakiwa liishe.kwa muda wa miaka minne.
Daraja hilo la Magufuli lenye urefu wa kilo mita 3.2 na barabara unganishi 1.66 kilo mita, ambalo ni la kimkakati kwa ajili ya maendeleo ya wananchi kwa kukuza uchumi wao.
Maoni
Chapisha Maoni