UJASUSI WA MEMBE WAUANGUSHA UPINZANI
LAZIMA tujue kuwa anguko la CHADEMA mwaka huu ni la kihistoria. Haijawahi kutokea tangu kuanza kwa Mfumo wa Vyama vingi mwaka 1992. Labda kwa wasiofahamu dhambi ya kumkataa Jasusi au Kachero (Membe) kwenye Chama hicho ndio mwanzo wa kujiangusha wenyewe. Membe hakuridhika kukataliwa na CHADEMA akaamua kwenda ACT - Wazalendo ili iwe route ya kuwavuruga wote wawili. Ubaya ulianzia wapi? Baada tu ya mazungumzo na Viongozi waandamizi wa CHADEMA na Membe kutokubaliana kwa kuwa Membe alionesha kuwa anakwenda kwenye Chama na CASH za kutosha lakini Viongozi hao waliona ni bora aliyepigwa risasi (Lissu) kwa kuwa wananchi watamuonea huruma. Alichofanya Membe baada ya kutemwa CHADEMA Kwa kuwa Membe alikosa njia ya kuingia na kuibomoa CHADEMA aliamua kujiunga na ACT Wazalendo ili kuwapasua vizuri wote wawili kwa pamoja na lengo la kwanza likatimia. CHADEMA na ACT Wazalendo walijikanyaga wapi? Siku ambayo Mgombea wa Urais wa CHADEMA Lissu alipoenda kwenye Mkutano Mkuu wa ACT Wazalendo na kuhutubia