TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU TAARIFA ILIYOTOLEWA NA AMNESTY INTERNATIONAL

 

Tarehe 12/10/2020 Shirika la AMNESTY INTERNATIONAL lilitoa taarifa kwa vyombo vya habari iliyojaa upotoshaji kuhusu Serikali ya Tanzania, kwamba inakandamiza ASASI za kiraia kwa kuziwekea utaratibu wa usajili, kuwachukuliwa hatua wanasiasa wa upinzani wanaovunja sheria za nchi kwa makusudi pamoja na wanaharakati wa mitandaoni.

Katika ripoti yao wamelenga kutetea baadhi ya makundi yanayohamasisha uvunjifu wa amani nchini pamoja na kueneza agenda ya mapenzi ya jinsia moja (ushoga).

Shirika hili ni moja ya Mashirika yanayotumiwa na mabeberu kuishambulia Serikali ya Tanzania na  Mhe. Rais Dkt.  John Pombe Magufuli.

Katika Ripoti hiyo Amnesty imepotosha katika mambo yafuatayo:-

1. Ripoti hiyo imetetea watumiaji wa mitandao ya kijamii hasa wale wanaotukana  na kuwakejeli viongozi wa Serikali pamoja na viongozi wa dini wanao kemea unyonyaji wa rasilimali za nchi na  kwa kiasi kikubwa ripoti hiyo imewatetea wanaohamasisha ushoga kwa kueleza kuwa kila mtu ana uhuru wa kueleza hisia zake bila kuingiliwa.

2. Ripoti hiyo imevitetea vyombo vya habari vinara kwa kutoa lugha zisizo na staha kwa Serikali na Viongozi wake (Magazeti na online TV), kuwa eti vyombo hivyo viachwe vifanye kazi yao bila kuingiliwa, kwa maana nyingine ni kuwa vyombo hivyo viachwe viendelee kupotosha umma pamoja na kutoa lugha za matusi dhidi ya Serikali na viongozi wake.

3. Pia shirika hilo la kibeberu linatoa maelekezo ya namna gani Serikali ya Tanzania ifanye kazi kwa matakwa ya Shirika hilo, yaani ni vichekesho.

Nimejiuliza sana kwanini siku  za hivi karibuni kumekuwa na utitiri wa matamko yasiyo na maana kutoka kwa  Mashirika ya kibeberu dhidi ya Serikali ya Tanzania juu ya masuala yasiyowahusu kabisa ila wanayatolea matamko tena yanayoegemea upande mmoja.

Kuna sababu lukuki zinazosababisha mashirika hayo ya kibeberu kuiandama Serikali ya Tanzania hasa kipindi cha awamu ya tano, kwa leo tutaangazia kwa ufupi moja ya sababu hizo;

--->Kwanza ripoti nyingi zinazotolewa na mashirika hayo pamoja na mawakala wao, zinaandaliwa na baadhi ya wanasiasa wapinga maendeleo hapa nchini. (Tukipata wasaa tutakuja kuwazungumzia aina hii ya wanasiasa na sababu zinazowapelekea kuandaa ripoti hizo).

--->Mtakumbuka kipindi Serikali ya awamu ya tano ilipoingia madarakani Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli alisimama kidete kulinda rasilimali za nchi yetu hasa madini yaliyo kuwa yanawanufaisha mabeberu kwa miongo kadhaa sasa na kuwaacha Watanzania katika lindi la umasikini. 

Nchi hizo hazikuwa tayari kuona Tanzania inazinduka katika usingizi wa miaka yote uliosababisha wao kutajirika. Utakumbuka sakata la makanikia lilivyokuwa, mpaka likawahusisha baadhi ya Watanzania tena wanasiasa mashuhuri kuwatete waziwazi wanyonyaji hao.

--->Kwa wafuatiliaji mnafahamu ni kwa jinsi gani Mashirika yasiyo ya kiserikali yanafadhiliwa na nchi za mabeberu kuendesha kampeni mbalimbali kama vile kuhamasisha mapenzi ya jinsia moja, utoaji wa elimu kwa wananchi inayohamasisha chuki miongoni mwa Watanzania, ila Serikali ya awamu ya tano ilipoingia madarakani iliweka utaratibu wa kusajili Mashirika hayo ili kujua madhumuni ya Taasisi hizo ili kuilinda jamii yetu dhidi ya agenda zao zinazovunja maadili na desturi za Kitanzania. 

Jambo hilo limezidi kuwakereketa na kuwaudhi Mabeberu kwani mipango yao imekwamishwa kwa kiasi kikubwa na Serikali hii ya awamu ya tano.

--->Kitendo cha Serikali  kuweka utaratibu mahususi kwa wamiliki wa vyombo vya habari vya mitandaoni (Online media) kimezidi kuwavuruga kabisa mabeberu kwani agenda zao sasa hazipati upenyo kwenye jamii ya watanzania, sasa hili suala ndiyo limewakera zaidi Mabeberu na kusababisha hasira zao kuzihamishia kwenye matamko yasiyo na msin…

Na, Kelvin Chilebo,

Mchambuzi wa masuala ya kisiasa Nchini Tanzania.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Manufaa ya Ushirikiano wa Tanzania na Kenya

BE AWARE, Robert Amsterdam is a Canadian Set to Plant Violence in African Countries.

LICHA YA AHADI KUWA WANGESHIRIKIANA, LISSU NA MEMBE KILA MMOJA ANAGOMBEA “KIVYAKE.”