Machapisho

Kampeni ya Mguu kwa Mguu iliyofanyika Kawe ni fedheha kwa CHADEMA, kwani Imekosa Mvuto kwa Wananchi

Picha
Jana nikiwa katika shughuli zangu za kila siku katika baadhi ya mitaa ya Jimbo la Kawe, nilibahatika kuona viongozi wa Chadema wakipita katika baadhi ya mitaa ya Jimbo la Kawe wakiendesha kampeni yao ambayo wameipa jina la Mguu kwa Mguu lengo likiwa ni kuwatembelea wananchi na kwahamasisha kukichangia chama hicho. Kwa kweli nilichokiona ni fedheha kwa Chadema kwani mwitikio wa wananchi ulikuwa mdogo sana katika kampeni hiyo tofauti na matarajio ya chama hicho licha ya kuamua kumtembeza mtaani Mbowe wakidhani kuwa italeta chachu ya kuwajaza watu wengi katika kampeni hiyo, cha ajabu ni kwamba wananchi walikuwa busy na shughuli zao bila shobo yoyote kwa Mbowe na genge lake lisilozidi watu 10 walio kuwa wakihaha mitaani peke yao bila kumbatana na nyomi ya wafuasi na wapambe wa Chadema kama ilivyozoeleka kipindi chama nyuma. Bila shaka Chadema walililenga Jimbo la Kawe wakijua ni ngome yao kama walivyozoea!!! Mazoea ya tabu…..Kawe ya sasa imebadilika siyo ile ya zamani…! Wananchi wako busy

CHADEMA Yalalamikiwa kupoteza Mvuto wa Kisiasa

Picha
''Mimi ni Mtanzania ninaishi nchini Marekani katika mji wa Chicago kiitikadi ni mfuasi wa CHADEMA, nimeguswa kuandika Makala hii kueleza masikitiko niliyonayo kwa vyama vya upinzani nchini hususani chama changu. Nianze na kusema kuwa CHADEMA kilikuwa ni chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania hakikuwa na mpinzani kilijikita kuikosoa Serikali na kutoa mawazo mbadala, kwa sasa hali imekuwa ya tofauti kwani CHADEMA wameshindwa kutimiza wajibu wao wa kukosoa na kutoa mawazo mbadala. CHADEMA kwa sasa hawana agenda wamebakia kudandia agenda za Serikali na chama Tawala CCM, yani nimekuwa nikifuatilia hawana wanachokifanya wamebakia tu kulalamikia mambo mbalimbali yanayofanywa na Serikali bila kutoa ushauri wa nini kifanyike. Naumia sana kuona chama changu kikishindwa kusimama katika nafasi yake, mpaka vyama vya wasaliti vilivyoanza juzi tu vinaanza kuleta upinzani. Najiuliza tatizo nini? Je ni mfumo wa uongozi? Je viongozi kutojua majukumu yao?  Hivi karibuni nimeshuhudia wanachadema

Manufaa ya Ushirikiano wa Tanzania na Kenya

Picha
  Tanzania na Kenya zimekubaliana kushirikiana kuondoa vikwazo vya biashara na kufungua milango Zaidi ya kuwekeza na kuinua uchumi baina ya nchi zote mbili. Makubaliano hayo yamefikiwa kufuatia Ziara ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan nchini Kenya ikiwa ni kuitikia mwaliko aliopewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyata. Ziara hiyo imekuwa na mafanikio makubwa kwa nchi zote Mbili kwani kuanzia Tarehe 05/05/2021 vikwazo vya Wafanyabiara wa Tanzania kuingiza mahindi nchini Kenya vimeondolewa. Pamoja na mafanikio hayo mambo mengine ya manufaa ni:- Kujenga na kuendeleza utamaduni wa kukutana mara kwa mara, hii itasaidia kutatua changamoto ndogondogo zinazojitokeza. Kushirikiana kwenye sekta ya utalii, kwamba badala ya kunyanganyana watalii busara itatumika kuwashawishi watalii kuongeza siku za kutembelea Kenya na Tanzania. Vyombo vya ulinzi kushirikiana kulinda maeneo yote ili kusaidia kuwepo kwa utulivu na kutoa fursa ya shu

Ujumbe wa Wakili Msomi kwa Wanaharakati wa Kenya

Picha
Kwanza ninaanza kwa kuwasalimia kwa salamu ya jina la Jumuiya ya Afrika Mashariki, poleni na hongereni kwa utekelezaji wa Majukumu yenu ya kila siku. Nimeguswa kuwatumia ujumbe wa wazi kufuatia ujumbe wenu mlioutoa kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu wa kumtaka awaachie huru wafugwa wa Kisiasa. Naelewa ujumbe wenu huu mmeutoa kufuatia Mhe. Rais Samia Suluhu kutoa Msamaha wa wafungwa 5001 siku ya maadhimisho ya miaka 57 ya Muungano wa Tanzania . Mmesema bado kuna wafungwa 200 wako Magereza kwamba mnamjulisha Mhe.Rais kwamba hajui!!!, Mhe. Rais anajua kila kinachoendelea nchini maana yeye ndiye Amiri Jeshi Mkuu, na anauwezo wa kuwaachia huru kama alivyofanya kwa wafungwa 5001, lakini uwezo huo alionao ni kwa mujibu wa sheria za nchi na siyo tu kwa mamlaka aliyonayo kama Rais. Mnapaswa kujua kuwa Wafungwa hao 5001 waliopewa msamaha na Rais kati yao 1516 wameachiwa huru baada ya kupunguziwa robo ya adhabu na Wafungwa 3,485 wamepunguziwa robo ya adhabu bada

WALICHOSEMA TEC NI USHAURI KAMA WALIVYOFANYA MWAKA 2020. TUSIPOTOSHE

Vyombo vya ndani na nje vimekuwa mstari wa mbele kupotosha waraka uliotolewa na Baraza la Maaskofu Tanzania ( TEC) kuhusu kujilinda na virusi vipya vinavyosababisha virusi vya corona vilivyogunduliwa Afrika ya Kusini na Uingereza. Wakati Baraza la Maaskofu likiwaomba watanzania kuchukua tahadhali kwa kuwa Tanzania sio kisiwa, vyombo vya habari vimesema Baraza limesema Tanzania kuna virusi hivyo vipya. Ukweli ni kwamba ukisoma waraka huo hauna tofauti kubwa na ule walioutoa mwaka 2020 mwezi wa pili ukiwaomba watanzania kuchukua tahadhali. Ikumbukwe kuwa dini na viongozi wote wa imani wanalo jukumu la kuwakumbusha waumini kutenda na kuishi maisha mema. Hili ndo walilofanya Baraza la Maaskofu kuwakumbusha waamini wao na watanzania kwa ujumla kutokubweteka na kuendelea kufuata miongozo iliyotolewa na wizara ya afya ya kunawa mikono, kuvaa barakoa, kuepuka misongamano isiyo ya lazima na mingine mingi. Ni kwa msingi huo ukisoma waraka huo hakuna popote unaposema Tanzania kuna virusi vipya vi

Barua ya Wazi kwa Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula

Picha
Amani iwe kwako! Mimi nikiwa kama muumini wa Kanisa lako la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki nimeshangazwa na ujumbe ulioutuma katika barua ya wazi kwa Mhe.Rais Dkt John Pombe Magufuli kwani umeacha jukumu la msingi uliloitiwa na Mungu la kutuhubiria wananchi ili tuokoke na kumrudia Mungu. Inafikirisha kukuona Askofu wangu ukiacha majukumu yako na kuanza kufanya siasa, najiuliza huo wito aliopewa na Mungu ni kwa ajili ya kuhubiri neno au kufanya siasa? Nawaomba Mhe.Rais Magufuli pamoja na washauri wake na Watanzania kwa ujumla wenu muupuuze ujumbe huo  alioutoa kwani hauna nia njema ya kutujenga Wananchi zaidi ya kutugawa. Askofu wangu Mwamakula  umesema kuwa unataka kufanya "Matembezi ya Hiyari" nchi nzima yenye lengo la kuuhamasisha Umma wa Tanzania kuhusu Kuunda Tume Huru ya Uchaguzi na Kuandika Katiba Mpya. Najiuliza tu hivi nilishawahi kukusikia au kukuona ukifanya  matembezi ya hiyari kuhamasisha watu kumjua Mungu na kuokoka? Jibu ni hapana!.  Kwanini

Aliyegombea Ubunge Jimbo la Siha kupitia Chadema Elvis Christopher Mosi Atimukia CCM

Picha
Wakati Tukielekea Kuupokea Mwaka 2021 Leo Aliyekuwa Mgombea Ubunge Jimbo la Siha Kwa Tiketi Ya Chadema Kamanda ELVIS CHRISTOPHER MOSI Leo Amemwaga Manyanga na Kujiunga Na Chama Cha Mapinduzi. Aidha, Ndugu ELVIS CHRISTOPHER MOSI  Ameamua Kujiunga na Chama Cha Mapinduzi Kutokana na Sera za Chama Cha Mapinduzi Zilizojikita Katika Kuleta Maendeleo Kwa WaTanzania. Sambamba na Zoezi Hilo Pia Aliyekuwa Katibu Wa Chadema Wilaya ya Siha na Mjumbe wa Baraza Kuu Chadema Taifa Kamanda Emanuel Nabora Amestaafu Siasa na Kuachana Na Nafasi Zake Zote Ndani Ya Chadema.