Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili, 2022

Kampeni ya Mguu kwa Mguu iliyofanyika Kawe ni fedheha kwa CHADEMA, kwani Imekosa Mvuto kwa Wananchi

Picha
Jana nikiwa katika shughuli zangu za kila siku katika baadhi ya mitaa ya Jimbo la Kawe, nilibahatika kuona viongozi wa Chadema wakipita katika baadhi ya mitaa ya Jimbo la Kawe wakiendesha kampeni yao ambayo wameipa jina la Mguu kwa Mguu lengo likiwa ni kuwatembelea wananchi na kwahamasisha kukichangia chama hicho. Kwa kweli nilichokiona ni fedheha kwa Chadema kwani mwitikio wa wananchi ulikuwa mdogo sana katika kampeni hiyo tofauti na matarajio ya chama hicho licha ya kuamua kumtembeza mtaani Mbowe wakidhani kuwa italeta chachu ya kuwajaza watu wengi katika kampeni hiyo, cha ajabu ni kwamba wananchi walikuwa busy na shughuli zao bila shobo yoyote kwa Mbowe na genge lake lisilozidi watu 10 walio kuwa wakihaha mitaani peke yao bila kumbatana na nyomi ya wafuasi na wapambe wa Chadema kama ilivyozoeleka kipindi chama nyuma. Bila shaka Chadema walililenga Jimbo la Kawe wakijua ni ngome yao kama walivyozoea!!! Mazoea ya tabu…..Kawe ya sasa imebadilika siyo ile ya zamani…! Wananchi wako busy