CHADEMA Yalalamikiwa kupoteza Mvuto wa Kisiasa
''Mimi ni Mtanzania ninaishi nchini Marekani katika mji wa Chicago kiitikadi ni mfuasi wa CHADEMA, nimeguswa kuandika Makala hii kueleza masikitiko niliyonayo kwa vyama vya upinzani nchini hususani chama changu. Nianze na kusema kuwa CHADEMA kilikuwa ni chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania hakikuwa na mpinzani kilijikita kuikosoa Serikali na kutoa mawazo mbadala, kwa sasa hali imekuwa ya tofauti kwani CHADEMA wameshindwa kutimiza wajibu wao wa kukosoa na kutoa mawazo mbadala. CHADEMA kwa sasa hawana agenda wamebakia kudandia agenda za Serikali na chama Tawala CCM, yani nimekuwa nikifuatilia hawana wanachokifanya wamebakia tu kulalamikia mambo mbalimbali yanayofanywa na Serikali bila kutoa ushauri wa nini kifanyike. Naumia sana kuona chama changu kikishindwa kusimama katika nafasi yake, mpaka vyama vya wasaliti vilivyoanza juzi tu vinaanza kuleta upinzani. Najiuliza tatizo nini? Je ni mfumo wa uongozi? Je viongozi kutojua majukumu yao? Hivi karibuni nimeshuhudia wanachadema