Ujumbe wa Wakili Msomi kwa Wanaharakati wa Kenya

Kwanza ninaanza kwa kuwasalimia kwa salamu ya jina la Jumuiya ya Afrika Mashariki, poleni na hongereni kwa utekelezaji wa Majukumu yenu ya kila siku.

Nimeguswa kuwatumia ujumbe wa wazi kufuatia ujumbe wenu mlioutoa kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu wa kumtaka awaachie huru wafugwa wa Kisiasa.

Naelewa ujumbe wenu huu mmeutoa kufuatia Mhe. Rais Samia Suluhu kutoa Msamaha wa wafungwa 5001 siku ya maadhimisho ya miaka 57 ya Muungano wa Tanzania.

Mmesema bado kuna wafungwa 200 wako Magereza kwamba mnamjulisha Mhe.Rais kwamba hajui!!!, Mhe. Rais anajua kila kinachoendelea nchini maana yeye ndiye Amiri Jeshi Mkuu, na anauwezo wa kuwaachia huru kama alivyofanya kwa wafungwa 5001, lakini uwezo huo alionao ni kwa mujibu wa sheria za nchi na siyo tu kwa mamlaka aliyonayo kama Rais.

Mnapaswa kujua kuwa Wafungwa hao 5001 waliopewa msamaha na Rais kati yao 1516 wameachiwa huru baada ya kupunguziwa robo ya adhabu na Wafungwa 3,485 wamepunguziwa robo ya adhabu badala ya punguzo la kawaida la theluthi moja na wataendelea kutumikia sehemu ya kifungo iliyobaki. Swali la kujiuliza ni hao mnaotaka waachiwe huru wametimiza matakwa hayo ili msamaha mwingine wa Rais waachiwe? Maana hakuna msamaha wa Rais kama vigezo vya kuachiwa havijatimizwa.

Mmesema kuwa watanzania waliowatuma Mmwambie Rais Samia katika ziara aliyofanya nchini Kenya, eti kwa madai kuwa huku Tanzania kuna ugumu wa kusikilizwa, Hakuna ugumu huo mnaoaminishwa na hao wachache kwa sababu suala la msamaha ni la kisheria siyo matakwa ya Rais.

Ushauri wangu kwenu ni kuwa mnapaswa kutambua kuwa huku kwetu Tanzania tuna Mihimili mitatu ya SERIKALI ambayo utendaji kazi wake hauingiliani yani kila muhimili unajitegemea katika utawala na utekelezaji wa majukumu yake.

Muhimili wa kwanza ni SERIKALI ni mamlaka ya utendaji inayotekeleza sheria, Serikali hii ndiyo inaogozwa na Rais Mhe. Samia Suluhu, wa pili ni BUNGE ambalo ni mamlaka ya kutunga sheria, muhimili huu unaongozwa na Spika wa Bunge ambaye ni Job Ndugai na wa tatu ni MAHAKAMA ambayo ina mamlaka ya kuamulia sheria unaongozwa na Jaji Mkuu Ibrahimu Juma.

Hao wafungwa mnaoshinikiza waachiwe huru wako kwenye muhimili wa Mahakama Mhe. Rais hausiki nao kilichopo ni taratibu, kanuni na sheria ndizo zinzoweza kutumika kuwafanya kuwa huru na siyo Mhe. Rais. Nawashauri mnapopaza sauti zenu mtambue hilo ili msiendelee kumtwisha Rais majukumu ambayo Hayapo kwenye utawala wake. Mjue tu kuwa hata hao wafungwa 5001 walioachiwa huru siku ya Muungano wameachiwa kwa mujibu wa kanuni, Taratibu na sheria za Mahakama.

Mwisho niseme tu Mahakama Tanzania iko huru haifanyi kazi kwa Mashinikizo inaogozwa kwa SHERIA.

By Isdor Ndigo

Wakili wa kujitegemea na Mtetezi wa Haki za Binadamu.




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

BE AWARE, Robert Amsterdam is a Canadian Set to Plant Violence in African Countries.

DAVID KAFULILA APANGUA HOJA 7 ZA TUNDU LISSU KWA TAKWIMU