WALICHOSEMA TEC NI USHAURI KAMA WALIVYOFANYA MWAKA 2020. TUSIPOTOSHE


Vyombo vya ndani na nje vimekuwa mstari wa mbele kupotosha waraka uliotolewa na Baraza la Maaskofu Tanzania ( TEC) kuhusu kujilinda na virusi vipya vinavyosababisha virusi vya corona vilivyogunduliwa Afrika ya Kusini na Uingereza.

Wakati Baraza la Maaskofu likiwaomba watanzania kuchukua tahadhali kwa kuwa Tanzania sio kisiwa, vyombo vya habari vimesema Baraza limesema Tanzania kuna virusi hivyo vipya.

Ukweli ni kwamba ukisoma waraka huo hauna tofauti kubwa na ule walioutoa mwaka 2020 mwezi wa pili ukiwaomba watanzania kuchukua tahadhali.

Ikumbukwe kuwa dini na viongozi wote wa imani wanalo jukumu la kuwakumbusha waumini kutenda na kuishi maisha mema.

Hili ndo walilofanya Baraza la Maaskofu kuwakumbusha waamini wao na watanzania kwa ujumla kutokubweteka na kuendelea kufuata miongozo iliyotolewa na wizara ya afya ya kunawa mikono, kuvaa barakoa, kuepuka misongamano isiyo ya lazima na mingine mingi.

Ni kwa msingi huo ukisoma waraka huo hakuna popote unaposema Tanzania kuna virusi vipya vinavyosababisha corona au virusi vya zamani.

Hii yote inatokana na tabia iliyozuka siku za karibuni ya vyombo vya habari kuacha misingi ya weledi ya kazi zao ya kusoma mstari kwa mstari kila chapisho litolewalo na kupotosha jamii.

Watanzania waache upotoshaji huu wa vyombo vya habari kuhusu tamko la baraza la Maaskofu waendelee kuchukua tahadhari kama serikali inavyoshauri.

Ikumbukwe kuwa pamoja na kuwa Tanzania hamna COVID-19, serikali haijawahi kuwaambia wananchi kuacha kunawa mikono, kuvaa barakoa au kuwa katika misongamano isiyo na umuhimu.

Siku zote serikali imesisitiza Watanzania kuendelea kutomjaribu Mungu na kuchukua tahadhali zote dhidi ya COVID-19 baada ya Mungu kuiondoa Tanzania.

Kwa mantiki hii Watanzania wapuuze vyombo vya habari vya nje na ndani pamoja na mitandao ya kijamii iliyopotosha waraka wa Maaskofu.

Sambamba na hilo,  Watanzania wapuuze vyombo hivihivi vilipotosha alichosema Waziri wa fedha Dr. Philipo Mpango wakati akiongea na wafanyakazi wa wizara hiyo.

Dr. Mpango amesema pamoja na kuwa Tanzania hamna COVID-19 wafanyakazi wachukue tahadhali kwani Tanzania sio kisiwa.

Kama kawaida vyombo vya habari vikapotosha na kusema Tanzania kuna COVID-19 kulingana na maelezo ya Dr. Mpango.

Watanzania tuendelee kuwa watulivu na kuisikiliza Wizara ya Afya yenye dhamana ya kulinda afya zetu.

Serikali yetu ni sikivu likitokea lolote itatwambia ila sio porojo zinazochagizwa na vyombo vya habari na mitandao ya kijamii isiyofuata maandili ya uandishi wa habari

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Manufaa ya Ushirikiano wa Tanzania na Kenya

BE AWARE, Robert Amsterdam is a Canadian Set to Plant Violence in African Countries.

LICHA YA AHADI KUWA WANGESHIRIKIANA, LISSU NA MEMBE KILA MMOJA ANAGOMBEA “KIVYAKE.”