SIKU YA WAZEE DUNIANI, UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM KWA WAZEE
Tukiwa tunaadhimisha Siku ya Wazee Duniani ni vyema tukakumbushana juu ya Sera ya Taifa kwa Wazee.
Yaliyotekelezwa kwa Wazee Mwaka 2015 - 2020
Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Chama Cha Mapinduzi kiliendelea kuisimamia Serikali kutekeleza Sera ya Taifa ya Wazee ambapo mafanikio yafuatayo yamepatikana:-
(a) Kuongezeka kwa idadi ya wazee waliopatiwa vitambulisho vya kuwawezesha kupata matibabu bila malipo kutoka 213,025 mwaka 2015 hadi kufikia wazee 1,042,403 mwaka 2020.
(b) Wazee na wasiojiweza 2,135 wanaoishi katika makazi 16 yanayomilikiwa na Serikali walipatiwa huduma za msingi za chakula, malazi, mavazi na matibabu kati ya mwaka 2015 na 2020.
(c) Kuimarisha upatikanaji wa huduma za afya kwa Wazee kwa kuanzisha madirisha 2,335 ya kutolea huduma za afya kwa wazee katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini.
(d) Kuanzishwa kwa mabaraza ya wazee 8,183 ili kuongeza wigo wa upatikanaji wa haki kwa wazee.
(e) Kudhibiti mauaji ya wazee kwa kutekeleza Mkakati wa Kutokomeza Mauaji ya Wazee.
(f) Kuboresha makazi ya wazee kwa kukarabati na kujenga miundombinu mipya katika makazi ya wazee ya Kolandoto (Shinyanga), Nunge (Dar es Salaam), Njoro (Kilimanjaro), Magugu (Manyara) na Fungafunga (Morogoro).
Yatakayotekelezwa kwa Wazee Mwaka 2020 - 2025
Katika kuimarisha utoaji wa huduma za ustawi wa jamii kwa wazee, katika kipindi cha miaka mitano ijayo, CCM itaekekeza Serikali kuchukua hatua zifuatazo:-
(a) Kuimarisha huduma za matibabu bila malipo kwa wazee.
(b) Kuimarisha huduma za msingi kwa wazee wasiojiweza nchini katika makazi ya wazee yanayomilikiwa na kuendeshwa na Serikali pamoja na sekta binafsi.
(c) Kukarabati na kujenga miundombinu katika makazi ya wazee.
(d) Kuendeleza utekelezaji wa Mkakati wa Kutokomeza Ukatili na Mauaji ya Wazee.
(e) Kutoa huduma za matunzo na kisaikolojia kwa wazee na watu wenye ulemavu.
(f) Kuimarisha mabaraza ya wazee maeneo yote nchini.
(g) Kuongeza wigo wa mafao kwa wazee.
#ChaguaMagufuli kwa Ustawi wa Wazee wetu
#SikuyaWazeeDuniani.

Maoni
Chapisha Maoni