LISSU USIPOTOSHE, UJENZI WA UWANJA WA NGEDE CHATO NI MUHIMU KWA TAIFA



Nimekuwa nikifuatilia kwa ukaribu kampeni za Urais zinazoendelea Nchini, jana nilimsikia mgombea wa Urais wa CHADEMA TUNDU LISSU akijinadi kwa kubeza jitihada zilizofanywa na Serikali katika kujenga Uwanja wa Ndege wa Chato, Mkoani Geita.

Kabla ya Kuanza kujadili kwa kina kuhusu tija ya uwanja huo, ni AIBU kwa mgombea wa nafasi ya Urais kubeza suala la ujenzi wa kiwanja cha Ndege na kuifanya kuwa ajenda kuu ya kumuingiza Ikulu, katika hali ya kawaida tulitarajia mgombea wa nafasi ya Urais wa upinzani kuja na Sera mbadala kabambe na madhubuti za kiuchumi, kisiasa na kijamii ili kuvuta hisia za wapiga kura.

Turejee kwenye mjadala wetu mama wa ujenzi wa uwanja wa Ndege Chato, nilichobaini katika mijadala mingi inayoendelea kuhusu jambo hilo ni wachangiaji wengi wanaongozwa na mihemko na itikadi za kisiasa bila kuwa na tafakuri ya kina ili kubaini uhalisia wa jambo hilo.

Ili kuwa na uelewa  wa pamoja, kwa nini ujenzi huo ulifanyika Chato ni muhimu tukafahamu mambo  machache kuhusu Chato, Geita na Maeneo jirani, kama ifuatavyo:-

● Kijiografia Mji wa Chato upo karibu zaidi na hifadhi za Taifa za Burigi, Ibanda, Kimisi, Rumanyika na Biharamulo ambazo zote zinapatikana Mkoa wa Kagera. Vilevile upo karibu sana na hifadhi ya Rubondo yenye wanyama mbalimbali kama Twiga, Tembo, Swala, Viboko, Pongo na Sokwe mtu.


● Wilaya ya Chato inapatikana katika mkoa wa Geita ambao una Mgodi mkubwa wa Geita Gold Mine (GGM) uliochini ya muwekezaji na umekuwa ukitajwa kuwa miongoni mwa migodi ambayo inauzalishaji mkubwa wa dhahabu barani Afrika. Kadhalika ndani ya Chato kuna shughuli za uchimbaji madini zinazofanywa na wachimbaji wadogo katika maeneo ya Msasa, Matabe, Imwelu, Makurugusi, Bwanga, Iparamasa, Buseresere na Nyarutembo 

● Wilaya ya Chato inapatikana karibu na Ziwa Victoria lenye samaki wa aina mbalimbali ikiwemo Sato, Sangara, Mumi, Dagaa, Gogogo na Kamongo.

Baada ya kupata wasifu mfupi wa Wilaya ya Chato, Mkoa wa Geita kwa ujumla na maeneo jirani, kwa mtazamo wa jicho la kiuchumi hasa uchumi wa kati tulioufikia, ujenzi wa uwanja wa ndege wa Chato ni wa kimkakati na utakuwa na manufaa yafuatatyo;-

i) Kuongeza idadi ya watalii katika hifadhi ya Taifa ya Lubondo Mkoani Geita na hifadhi zilizopo Mkoani Kagera kwa kuwa kiungo muhimu kati ya Tanzania na Nchi jirani za DRC Congo, Burundi, Rwanda na Uganda ambazo ni jirani kabisa na vivutio husika. Hivyo kuiongezea Serikali mapato.

ii) Utasaidia kuongeza na kuimarisha usafirishaji wa abiria kwenda Nchi jirani, mizigo, mazao na bidhaa mbalimbali kama vile asali, minofu ya samaki kutoka Tanzania kwenda nje ya Nchi.

iii) Utachangia katika kutoa ajira kwa vijana, kukuza biashara katika wilaya ya Chato na Mkoa wa Geita kwa ujumla hivyo kusababisha Watanzania kuondokana na umasikini.

iv) Utasaidia kuongeza ushirikiano wa kibiashara na kiuchumi kati ya Tanzania na Mataifa jirani ya Uganda, DRC Congo, Rwanda na Burundi.

Kwa ujumla kiwanja hicho kitakuwa na tija katika maeneo ya Utalii, biashara na katika sekta za kilimo, uvuvi na ufugaji. Pia utasaidia kuibua vivutio vingine vya utalii vitakavyovutia watalii wengi zaidi kuitembelea Tanzania.

Ni muhimu ikafahamika kwamba, kando na ujenzi wa uwanja wa ndege wa Chato, Serikali ya Awamu ya Tano inajenga uwanja wa Kisasa wa Msalato Dodoma na imeimarisha miundombinu ya majengo ya kupumzikia abiria, imepanua barabara ya kutua na kuruka ndege katika viwanja vya Iringa, Mwanza, Dodoma, Mpanda Mkoani Katavi, Bukoba Mkoani Kagera, Tabora na Arusha.

Kutokana na faida za kiuchumi na Kijamii za Uwanja huo inashangaza sana kusikia baadhi ya watanzania wanajenga hoja dhaifu kwamba Mhe.Rais anapendelea Chato kwa kuwa ndiyo nyumbani kwao, Watanzania tujiulize hivi Kata, Wilaya, Mkoa au Kanda ikitoa kiongozi wa juu Serikalini Wananchi wa eneo hilo HAWANA HAKI ya kupelekewa maendeleo hadi kiongozi huyo atoke madarakani??. 

Watanzania tubadilike kwa kuachana na fikira hizo potofu, wakazi wa Chato kama sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wana haki ya kupelekewa maendeleo kama wananchi wa maeneo mengine.

Bariki Kimaro

Mchumi & Mwanaharakati wa Maendeleo 

Rombo, Kilimanjaro 

16.10. 2020

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Manufaa ya Ushirikiano wa Tanzania na Kenya

BE AWARE, Robert Amsterdam is a Canadian Set to Plant Violence in African Countries.

LICHA YA AHADI KUWA WANGESHIRIKIANA, LISSU NA MEMBE KILA MMOJA ANAGOMBEA “KIVYAKE.”