MTEGO WA ZITTO KABWE WAINASA CHADEMA DAKIKA ZA MWISHO



Habari wafuatiliaji na wapenzi wa siasa za Tanzania.

Leo tutaanzia nyuma kidogo mwaka 2013 kipindi ambacho Zitto Kabwe alijiengua wadhifa wake wa  Unaibu Katibu Mkuu wa Chama cha Deokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kueleza kuwa yeye hatojitoa CHADEMA kwa ridhaa yake ila kama CHADEMA wataamua kumfukuza basi ataondoka.

Kipindi hicho kulikuwa na minong’ono mingi kumuhusu Zitto Kabwe kwamba ni msalti wa chama chao, mara anatumiwa na CCM kuihujumu CHADEMA mara wengine wakamtetea na kueleza kuwa ni njia za kumdhibiti ili asigombee nafasi ya uenyekiti wa chama hicho. Anyway, CHADEMA na Zitto Kabwe wanaelewa undani na ukweli wa mambo hayo.

Baada ya purukushani hizo zote, zilisababisha Zitto Kabwe kuanzisha chama chake cha ACT Wazalendo, ambapo nadhani ilikuwa ni smart move kwake. 

Hivi karibuni wakati wa mchakato huu wa kuelekea Uchaguzi Mkuu tulisikia tetesi nyingi kuhusu Vyama vya upinzani kuungana ili kumsimamisha mgombea mmoja wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuachiana baadhi ya majimbo kwa upande wa Ubunge na Kata kwa upande wa Udiwani. Ila kila chama kilikuwa kikihofia muungano huu kwa kuwa Vyama hivi vinakumbukumbu nzuri kabisa kuhusu muungano wao wa mwaka 2015 maarufu kama UKAWA ulivyo vikwamisha.

Wakati wa UKAWA kuna vyama hususan CHADEMA vilifaidi muungano huo na kuviacha vyama vingine vikiwa na mshangao mkubwa. Sasa hii ndiyo ilikuwa changamoto kubwa kwa vyama vya upinzani kuungana kwenye uchaguzi wa mwaka 2015.

Kipindi hiki Zitto Kabwe ametumia akili nyingi sana kuucheza mchezo huo huo bila kuonekana, amewaweka CHADEMA kwenye mtego ambao umewanasa bila kujua kama ni mtego wa makusudi.

Kwanza kabisa mtakumbuka kipindi ambacho Tundu Lissu alipokuwa hospitali Nairobi na Ubelgiji Zitto Kabwe alikuwa mtu ambaye anamjulia hali mara kwa mara na kuonekana kuwa na mazungumzo kati yao yaliyo ashiria kuwa huenda Zitto Kabwe anamshawishi Tundu Lissu kujiunga na chama chake, jambo ambalo halikufanikiwa baada ya Freeman Mbowe kumpa Tundu Lissu cheo cha Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA. Hilo lilimpa ugumu Tundu Lissu kuhamia ACT Wazalendo na huo ndio ulikuwa mtego wa kwanza wa Zitto Kabwe kwa CHADEMA ambao CHADEMA waliung’amua mapema.

Baada ya Zitto Kabwe kuona mtego huo umeangukia patupu alikuja na mpango kabambe wa “coalition” ambapo alitumia mitandao ya kijamii kuvishawishi vyama makini vya upinzani kuungana na kuwa na mgombea mmoja wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huku mipango ya kumshawishi Benard Membe kuhamia ACT Wazalendo ikiwa inaendelea. Hapa CHADEMA walitafakari kwa kina na wakaanza mazungumzo ambayo sina uhakika kama yalifika muafaka mzuri kama Zitto Kabwe alivyokuwa akitegemea.

Baada ya Benard Membe kuhamia ACT Wazalendo, ZITTO KABWE aliendelea kusisitiza muungano wa vyama vya upinzani akitegemea kuwa Benard Membe atapendekezwa kuwa mgombea anayeungwa mkono na vyama hivyo jambo ambalo CHADEMA walikataa na kumsimamisha mgombea wao. Huu mtego pia CHADEMA waliuvuka salama.

Sasa hali imekuwa mbaya kwa chama cha ACT Wazalendo baada ya Benard Membe kuacha kufanya kampeni kutokana na kuona hana ushawishi kwa Watanzania, mpaka viongozi wa chama hicho kutamka hadharani kuwa wanamuunga mkono Tundu Lissu. 

Baada ya Zitto Kabwe kuona mitego yake yote inaangikia patupu na akikumbuka kilichomtokea kipindi yupo CHADEMA roho inamuuma, sasa amekuwa ni mtu ambaye yupo nyuma ya Benard Membe.

Mchezo upo hivi, Zitto Kabwe ana hasira na CHADEMA tangu mwaka alipoondoka ndani ya chama hicho, sasa amesimama na Benard Membe kuwagawa wapiga kura upande wa Tundu Lissu huku akimwacha Benard Membe kuendelea na kampeni ili walau wapate nafasi ya kupata nafasi kadhaa za Ubunge viti maalum pamoja na Wabunge na Madiwani.

Kwa upande wa Zanzibar, Zitto amefanikiwa kuwashawishi CHADEMA kuwaachia wagombea wa ACT Wazalendo Zanzibar. Kwa maana nyingie ni kuwa CHADEMA hawana chao kwa upande wa Zanzibar na huku bara Zitto Kabwe anawaporomosha kwa kumtumia Benard Membe, na baadhi ya  wagombea ubunge wake ambao wameanza kung’ang’ania majimbo ambayo CHADEMA waliachiwa kuweka wagombea. 

Zitto na Seif ni wasanii na wanajua wanachokitafuta ndiyo maana wakisimama majukwaani wanaeleza kuwa watampigia kura Tundu Lissu ila wakishuka majukwaani wanamwambia Benard Membe aendelee kupambana ili kupunguza kura za CHADEMA. Mtego huu, CHADEMA wamechelewa sana kuugundua, na naamini uchambuzi wangu ndiyo utakaowafungua akili ya kuelewa kinachoendelea.

Huyo ndiyo Zitto Kabwe na chama chake.

Maoni

  1. Takataka tupo, unapoteza muda kuandika ushuuzi Kama huu

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Manufaa ya Ushirikiano wa Tanzania na Kenya

BE AWARE, Robert Amsterdam is a Canadian Set to Plant Violence in African Countries.

LICHA YA AHADI KUWA WANGESHIRIKIANA, LISSU NA MEMBE KILA MMOJA ANAGOMBEA “KIVYAKE.”