KISHERIA ACT HAINA MGOMBEA URAIS ZANZIBAR WALA ZITO SI MBUNGE WA ACT TENA
Na Mwamba wa Kaskazini
Jamaa mmoja aliwahi kuniambia sikia tu kitu inaitwa utawala bora au imba sana kuhusu hiyo kitu lakini ukiwa wewe ndio unatakiwa kutekeleza hapo kwa wengi vumbi kubwa hutimka.
Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe na Mgombea wake huko Zanzibar Maalim Seif Sharrif Hamad wamekosa sifa za kuendelea kuongoza na hata kuwa wagombea wa chama hicho.
Hii inakuja kufuatia Ibara ya 11(4) ya Katiba ya Chama hicho Toleo la 2015 kusisitiza wazi kuwa mtu atakoma kuwa mwanachama wa ACT Wazalendo iwapo atatangaza kuunga mkono mgombea wa Chama kingine wakati chama hicho kimeweka mgombea.
Kwa kauli hii ya Katiba na kitendo cha sasa cha Zitto na Maalim Seif kutangaza hadharani kuwa wanamuunga mkono mgombea wa CHADEMA wa Urais, Tundu Lissu, wakati Chama hicho cha ACT bado kina mgombea wake wa Urais, Ndugu Bernard Membe.
Kwa Katiba hiyo Maalim Seif amekoma kuwa mwanachama wa ACT na hivyo anakosa sifa za kugombea Urais wa Zanzibar. Zitto pia anaanguka kuwa mwanachama wa CHADEMA na hivyo anapoteza nafasi zote za uongozi kwenye chama hicho.
Sasa swali ni Je, wataenzi misingi ya utawala bora kwa kuenzi Katiba yao inavyosema na kujiengua katika nafasi na kinyang'anyiro wanachoshiriki?

Maoni
Chapisha Maoni