TUNDU LISSU ALIVYOIGHARIMU CHADEMA KISIASA NA KIUCHUMI KUELEKEA 2025

 Kwanza kabisa mtakumbuka kipindi ambapo Zitto Kabwe alimshawishi Tundu Lissu kujiunga na chama cha ACT Wazalendo kwa kumuahidi kumpendekezwa kuwa mgombea Urais kupitia chama hicho, jambo ambalo Mbowe alilitambua mapema  na kuamua kumpa cheo cha Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, hivyo Lissu akashindwa kutimkia ACT Wazalendo na kuamua kuukwaa Umakamu Mwenyekiti wa CHADEMA baada ya kuahidiwa kuwa mgombea Urais 2020.

Baada ya CHADEMA kumpa Lissu nafasi ya kugombea Urais kupitia chama hicho ndipo walipojipalia makaa ya moto vichwani mwao na hawakutegemea kuona mambo ambayo aliyafanya majukwaani wakati wa kampeni za uchaguzi, tuanze na kuyaangazia haya:-

Kwanza kabisa alifanya siasa za kujielezea yeye binafsi majukwaani hasa tukio lake la kupigwa risasi. Siku ya ufunguzi wa kampeni Lissu hakuongea kabisa sera za chama hicho bali alijikita kuelezea matatizo yake binafsi mpaka ikabidi siku ya pili ya kampeni Mbowe kumwomba ajikite kuelezea sera na sio mambo binafsi ila Lissu hakufanya hivyo, hali iliyopelekea Mbowe kususia mikutano ya kampeni za Lissu.

Pili, Lissu alijikita kutukana na kuisimanga Serikali hasa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli badala ya kueleza sera au kukinadi chama chake kwa wananchi hali ambayo imesababisha kushindwa kuzielewa sera za CHADEMA.

● Lissu alitumia muda mwingi kuwatisha watumishi wa Serikali kama vile IGP, Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi pamoja na viongozi wengine wa vyombo vya ulinzi na usalama kuwa atawashtaki ICC huku akiacha jukumu lake kuu  la kufanya kampeni na kukinadi chama chake kwa wananchi.


● Cha ajabu na cha kusikitisha kabla hata ya kupiga kura Lissu aliahidi kuwaingiza wafuasi wake barabarani kuandamana kupinga matokeo, hiyo ilikuwa dalili tosha  kudhihirisha kuwa Lissu aliona kuwa hawezi  kushinda uchaguzi.

Baadaya kushindwa uchaguzi akawahamasisha viongozi wa chama chake pamoja na Zitto Kabwe kufanya maandamano yasiyo na kikomo hilo nalo CHADEMA hawakuona kuwa ni mtego mwingine wa kuzidi kuporomoka kisiasa hasa pale maandamano hayo yalipokosa mwitikio wa wananchi.

● Kwa ujumla Lissu amechangia kwa asilimia kubwa CHADEMA kukosa wabunge kwa sababu alishindwa kuwanadi ipasavyo kwenye kampeni. Jambo ambalo hata viongozi wa chama wanajilaumu kwa kumsimamisha kugombea kwamba wangemsimamisha hata Mbowe labda wangepata wabunge wengi. Kwa sasa Lissu anaendelea kuwashawishi viongozi wa chama chake wasipeleke wabunge wa viti maalumu Bungeni kwa visingizio vya hovyo kabisa na Mbowe bado hajashtuka mpaka sasa.

Kuelekea mwaka 2025 Mbowe hatakuwa na fedha za ruzuku kutoka Serikalini, mshahara wa Ubunge wala marupurupu, kuwa kiongozi Mkuu wa Kambi rasmi ya Upinzai Bungeni (KUB) na zile fedha ambazo alikuwa akizichukua kila mwezi kutoka kwa wabunge wakuchaguliwa na wale wa viti maalum. Ameachiwa chama chenye mbunge mmoja tu bungeni, hii ni sawa na kusema amebaki na “chama mifupa’’, Baada ya kuvurugwa na kiongozi mwenzake aliyemwamini na kumpa nafasi ya uongozi wa juu na kumteua kugombea Urais.

Sasa Lissu amerudi kuzurura kwenye Mataifa ya Ulaya kwa Ufadhili wa Mataifa hayo kuisema vibaya Tanzania huku akilipwa mamilioni ya fedha, huku Mbowe akiendelea kupambana na hali yake hapa Nchini, akiwa hana hata chanzo chochote halali cha fedha kwa ajili ya chama chake.

Na hili ndiyo anguko la kisiasa na la kiuchumi la CHADEMA kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka 2025.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Manufaa ya Ushirikiano wa Tanzania na Kenya

BE AWARE, Robert Amsterdam is a Canadian Set to Plant Violence in African Countries.

LICHA YA AHADI KUWA WANGESHIRIKIANA, LISSU NA MEMBE KILA MMOJA ANAGOMBEA “KIVYAKE.”