WALIOKUWA WANATUMIWA NA MABEBERU KUICHAFUA TANZANIA WAANZA KUTOROKA NCHINI




Habari za muda huu wanafuatiliaji na wachambuzi wa masuala ya kisiasa hapa Nchini.

Kwa miaka kadhaa sasa kumekuwa na fununu na minong’ono ya chini chini kuwa baadhi ya wanasiasa wanatumiwa na Mataifa ya Nje kuishawishi na kuishinikiza Serikali kupitisha ama kutunga sera ambazo zinaweza kuyanufaisha Mataifa hayo huku wao wakipewa fedha pamoja na kuahidiwa hifadhi iwapo njama zao zitabainika na Serikali.

Tulishuhudia kipindi cha Makinikia baadhi ya wanasiasa hao akiwemo aliyekwa mgombea wa Urais kupitia CHADEMA Tundu Lissu walisimama kidete kuwatetea wanyonyaji wa rasilimali za Nchi yetu huku wakitishia kuwa Serikali itafunguliwa mashitaka kwa kitendo hicho cha kuzuia makinikia, na walifanya hivyo makusudi kwa kupewa maelekezo hayo na Mataifa hayo ili Serikali isiendelee kuzuia makinikia hayo.



Baadhi ya wanasiasa akiwemo Zitto Kabwe walioandika mpaka barua kwenye Taasisi za kifedha Duniani ili Tanzania inyimwe mikopo ya kuboresha Sekta ya Elimu Nchini, wengine walizunguka kwenye Mataifa hayo kuipaka matope Tanzania pamoja na Serikali yake, kazi hii walipewa na Mataifa hayo kwa sababu tu Serikali ya awamu ya Tano imeamua kusimamia rasilimali za Nchi ili kuwanufaisha wananchi wake.



Wanasiasa wengine ambao waliogozwa na Zitto Kabwe walipewa maelekezo ya kuendelea kupinga kila kazi inayofanywa na Serikali kwa kusema hayo sio maendeleo ya wananchi bali ni maendeleo ya vitu, na walijitahidi mno hasa kupitia mitandao ya kijamii na kwenye majukwaa ya kisiasa, tuliona mambo hayo katika ujenzi wa miundombinu, ufufuaji wa Shirika la ndege Nchini ATCL hata wengine wakibeza “Elimu bure”.

Ukiangalia hali ya kisasa kwa sasa hapa nchini utagundua kuwa yale waliyokuwa wakiyasema siku zote yanaendele kutimia, wapo wanasiasa ambao tayari wameshapewa hifadhi katika balozi za nchi hizo kama vile TUNDU LISSU ambaye ameshapewa hifadhi na ubalozi wa Ujerumani hapa nchini, GODBLESS LEMA ambaye alikamatiwa Nchini Kenya kwa kuingia bila kibali akiwa anaelekea Ubalozi wa Marekani nae akidai kutafuta hifadhi, Pamoja na LAZARO NYARANDU ambaye naye amekamatwa kwenye mpaka wa Namanga akielekea kuomba hifadhi Nchini kenya.




Wapo ambao tayari walishapatiwa hifadhi muda mrefu kama vile ANSBERT NGURUMO, EVARIST CHAHALI, DIDIER MLAWA pamoja na THOBIAS MARANDU, Wengine ambao wapo mbioni kwenda kutafuta hifadhi katika balozi au kwenda kuishi katika nchi hizo ni MARIA SARUNGI na baadhi ya watu wengine ambao wanatumiwa kuichafua nchi mitandaoni.

Watu hawa wote na washirika wao wamekuwa wakilipwa kutafuta, kukusanya, kuchambua na kuwakabidhi Mabalozi wa Nchi hizo taarifa nyeti za Nchi hii pamoja na kuwashauri mbinu mbalimbali za kilaghai na za kimikataba za kunyonya rasilimali za nchi yetu.

Kwa sasa Watanzania tunauelewa wa mambo haya ndiyo maana katika Uchaguzi huu hatujawachagua wanasiasa wote wanaotumiwa na Mabeberu kwa sababu wanahujumu Taifa mitandaoni na hata kwenye majukwaa ya kisiasa.

Wito wangu kwa Watanzania wa wapenda maendeleo wote, tuendelee kuwapuuza na kuwaangalia kwa jicho la kuwakataa watumwa wote wa mabeberu na tusiwape ushirikiano maana hawalitakii mema Taifa letu.



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Manufaa ya Ushirikiano wa Tanzania na Kenya

BE AWARE, Robert Amsterdam is a Canadian Set to Plant Violence in African Countries.

LICHA YA AHADI KUWA WANGESHIRIKIANA, LISSU NA MEMBE KILA MMOJA ANAGOMBEA “KIVYAKE.”