MPANGO WA MAANDAMANO YANAYORATIBIWA NA CHAMA CHA ACT WAZALENDO NA CHADEMA WAVUJA.
Raia Mwema.
Jioni hii baadhi ya viongozi wa CHADEMA kutoka mikoa tofauti, wamewasili Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya maandamano siku ya Tarehe 02/11/2020.
Lengo lao ni "kulianzisha" hapa Dar es Salaam ndipo baadae isambae mikoani. Mambo yaliyopangwa ni pamoja na kuchoma Matairi barabarani na kuleta vurugu za aina nyingi ili shughuli za kijamii zisimame.
Wamepanga mambo haya yaanze asubuhi ya siku ya Tarehe 02/11/2020 kwakuwa siku hiyo ni siku ya Kazi, hivyo lengo ni kufanya watu washindwe kwenda Makazini.
Pia vijana maalumu wataanzisha vurugu kwa ajili ya kufanya "looting" Kwenye sehemu za biashara. CHADEMA imegawagawa makundi Tofauti na haswa wamelenga Barabara zinazo ingia mjini, barabara inayo toka Kimara kuna vituo wameviweka na wata ziba kabisa njia. Pia Barabara za Mbagala, Tegeta na Barabara ya Banana (njia zote hizi zipo kwenye mpango wa kufungwa kabisa).
Aidha , kuna kundi moja la ACT WAZALENDO ambalo zamani walikuwa CUF na lipo maeneo ya Buguruni, kundi hilo limepewa kazi ya "kublock" Buguruni kwenye T-junction ( Makutano ya Barabara ya Uhuru na Mandela).
Viongozi wengi wa ACT WAZALENDO na wajumbe Wanne wa kamati kuu ya CHADEMA wamepinga mpango huo kuwa ni haramu kwa kuwa si makubaliano ya vikao halali vya Chama bali hasira za kushindwa Uchaguzi na hofu ya kukosa Ruzuku.
JESHI LA POLISI,
S.L.P 9140,
DAR ES SALAAM.
Maoni
Chapisha Maoni