HONGERA HALIMA MDEE NA WENZAKO KWA KUFUNGUA MINYORORO YA MFUMO DUME NA UBINAFSI NDANI YA CHADEMA


Kila Novemba 25 ulimwengu huaadhimisha Siku ya Kupambana na Ukatili Dhidi ya Wanawake, mwaka huu wa 2020 kauli mbiu inasema ''Ipake Dunia Rangi ya Chungwa: Nisikie Nami Pia. Kupinga Ukatili wa Kijinsia, Inaanza na Mimi.''

Maadhimisho ya siku hiyo nchini mwaka huu yamepambwa na tukio la kishujaa lililofanywa na Wanachama wa Bawacha wapatao 19 wakioongozwa na Mwenyekiti Taifa wa baraza hilo Halima Mdee walioamua kukataa ukatili dhidi yao wa kukatazwa na Uongozi wa CHADEMA wasiwakilishe jamii kubwa ya wanawake katika chombo muhimu cha kufanya maamuzi cha Bunge.

Kwa nini Taifa zima limewapongeza wabunge wa viti maalum wa Chadema kwa uamuzi huo? kwa Sababu haikuwa rahisi kwao kuvuka vikwazo vya mfumo dume na imani kwamba “wanaume wana sauti ya Mwisho kwenye maamuzi” hata ya wao kwenda kuapa kuwa wabunge licha ya kuwa ni haki yao kikatiba.

Viongozi wa Kitaifa wa CHADEMA (Wanaume) ni wabinafsi wanaojali maslahi yao, kwa sababu wao wanaendelea kuneemeka na fedha kutoka kwa mataifa ya nje, mathalani Tundu Lissu (amekuwa akipokea takribani dola elfu 3,500 kwa mwezi) Godbless Lema  amekuwa akilipwa zaidi ya dola 2,000 walitaka kuwanyima fursa wanawake hao ya kuwatumikia wananchi sanjari na kujipatia kipato cha kuweza kuendesha maisha yao ya kila siku.

Halima na wenzako mmefanya uamuzi sahihi na wa kizalendo unaolenga kuvunja mfumo dume na ubinafsi ndani ya Chadema. Nendeni Bungeni mkawasemee wanawake na wananchi kwa ujumla, historia itawakumbuka. Mtaitwa majina ambayo sio mapya kama wasaliti, vibaraka wapuuzeni hao wachache wasiopenda ukombozi wa jamii ya wanawake.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Manufaa ya Ushirikiano wa Tanzania na Kenya

BE AWARE, Robert Amsterdam is a Canadian Set to Plant Violence in African Countries.

LICHA YA AHADI KUWA WANGESHIRIKIANA, LISSU NA MEMBE KILA MMOJA ANAGOMBEA “KIVYAKE.”