WATANZANIA TUSIDANGANYIKE SERA YA SERIKALI YA MAJIMBO YA MGOMBEA URAIS WA CHADEMA TUNDU LISSU ITALIANGAMIZA TAIFA

Nimemsikia mgombea urais wa CHADEMA akinadi moja ya Sera yake ni kuanzisha mfumo wa Serikali za majimbo 

Ili tuwe na haki ya kumuunga mkono au kumpinga LISSU ni vyema tukajielimisha fasili ya  Serikali za majimbo na sababu zilizosababisha baadhi ya mataifa kuanzisha sera hiyo. 

Kimsingi kuna mifumo mikuu miwili inayotumika kuongoza Serikali Duniani kwa kimombo zinaitwa Unitary government na Federal government.

Katika mifumo hiyo miwili, tujikite kujadili mfumo wa Federal government ambao huzaa Sera ya Serikali ya majimbo inayoaahidiwa na LISSU.

Kwa mujibu wa taasisi ya International Institute for Democracy and Electoral  Assistance (IDEA) Federalism is a Constituonal mechanism for dividing power between different levels of government so that the federal units can enjoy Substantial,  Constitutionally guaranteed autonomy over certain Policy area while sharing power in accordance with agreed rules over other areas 

Kwa tafsiri isiyo rasmi, Federalism: ni mfumo wa kikatiba wa kugawa mamlaka katika ngazi mbalimbali za Serikali ambapo Serikali za majimbo hufurahia kuwa na mamlaka kamili ya Sera za eneo husika bila kuingiliwa na Serikali kuu.

Ndani ya mfumo wa Serikali ya Federalism mamlaka hugawanywa katika ngazi kuu mbili za (a) Kitaifa (national, Central or federal  (b) Majimbo (State, provincial or regional)

Jambo kuu la kuzingatia Serikali za majimbo hupewa mamlaka kamili ya kujiendeleza kimaendeleo kwa kutumia rasilimali zinazopatikana ndani ya jimbo husika.

Tanzania ya Serikali ya Majimbo itakuwaje? 

Tanzania itagawanywa katika majimbo kadri itakavyoonekana inafaa, naiona CHADEMA ikienda kucopy na kupaste mfumo wake wa kiutawala wa Sasa wa kanda,  na kuyaita majimbo na hivyo Tanzania itakuwa na majimbo 10 tu.

1. Jimbo Magharibi (Tabora, Katavi na Kigoma)

2.jimbo la Pwani( Dsm na Pwani)

3. Jimbo la Serengeti ( Mara, Simiyu na Shinyanga)

4.Jimbo  la Victoria ( Mwanza, Geita na Kagera)

5.Jimbo la Kaskazini (Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Tanga)

6.Jimbo la Kusini ( Mtwara, Lindi na Ruvuma)

7.Jimbo la kati (Dodoma, Singida, Morogoro)

8. Jimbo la Nyasa (Mbeya, Iringa, Njombe, Songwe na Rukwa)

9. Jimbo la Pemba (Kusini Pemba na Pemba Kaskazkni)

10. Jimbo la Unguja ( Mjini mabharibi, Kaskazkni Unguja na Unguja kusini)

Athari za mfumo huo zitakuwa ni pamoja na :-

(i) Kuongezeka kwa gharama za kuendesha Serikali kwa sababu ya ongezeko la idadi ya Ofisi, Watumishi. Rejea hali ilivyo Kenya.

(ii) Italeta ushindani wa kimaeneo wa uchumi uliojaa hujuma na kusababisha kuzuka kwa vikundi vya uasi dhidi ya Serikali kuu hivyo kuhatarisha umoja wa Kitaifa.

(iii) Utaongeza utofauti wa kimaendeleo ndani ya nchi mmoja,  majimbo yenye rasilimali nyingi za asili mfano jimbo la Kaskazini litaendelea kuneemeka zaidi

(iv)Itapunguza Uzalendo wa Taifa kwa sababu Wananchi watahamishia uzalendo wao kwa Serikali za majimbo.

(v) Itasabisha kuingiliana kwa majukumu kati ya Serikali kuu na Serikali za majimbo licha ya Katiba kujaribu kuweka mpaka wa majukumu ya Serikali hizo

(vi)Kuuingiza mhimili wa mahakama katika masuala ya kisiasa, migogoro mingi ya kimajukumu kati ya Serikali ya Jimbo na Serikali ya Kuu itahitaji Mahakama kutoa tafsiri ya majukumu badala ya Bunge kama ambavyo utamaduni wa Demokrasia unapendekeza.

(vii) Itapoteza haki za wachache 'potential exclusion of minorities'. Kuna uwezekano wa majimbo yenye kabila, lugha, utamaduni na dini moja yakashindwa kuheshimu tamaduni za wengine wachache.

Kwa mantiki hiyo Watanzania tukijichanganya tukachagua CHADEMA tumechagua Ukabila, Ukanda na utofauti wa Maendeleo nchini. 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Manufaa ya Ushirikiano wa Tanzania na Kenya

BE AWARE, Robert Amsterdam is a Canadian Set to Plant Violence in African Countries.

LICHA YA AHADI KUWA WANGESHIRIKIANA, LISSU NA MEMBE KILA MMOJA ANAGOMBEA “KIVYAKE.”