UFAFANUZI KUHUSU TAARIFA YA UPOTOSHAJI ULIOFANYWA NA BBC IDHAA YA KISWAHILI
1. Inashangaza kwa chombo chenye hadhi kimataifa kama BBC Swahili kuchukua taarifa kutoka mtaani na kuzirusha bila kupata uthibitisho toka kwa mamlaka husika.
2. Mkataba wa Serikali na Barrick sio wa siri.
3. Mkataba huo tangu usainiwe mwezi Januari mwaka 2020 haujawahi kubadilishwa.
4. Hakuna mkataba uliosainiwa mwaka 2017. Mwaka huo ndipo mazungumzo yalipoanza baada ya pande zote kusaini Statement of Undertakings.
5. Misingi muhimu ya kulinda maslahi ya Nchi imeendelea kuwa kama ifuatavyo:-
-> Madini yatachenjuliwa Tanzania na viwanda hivyo vimeanza kujengwa na Barrick wametenga dola milioni 5 kwa ajili ya kutafiti kuhusu ujenzi wa Smelter.
-> Baada ya kujenga Smelter hakuna madini ghafi yatasafirishwa. Hii ikihusisha pia madini mengine kama almasi na tanzanite.
-> Mapato yapatikanayo na mauzo ya madini yatahifadhiwa katika benki zilizopo Nchini na tayari Barrick wamekwishafungua akaunti Nchini na kufunga akaunti zilizokuwa nje ya Nchi. Matokeo ya hatua hizo ni kupanda kwa mchango wa sekta ya madini kwa asilimia 52 katika ongezeko la hifadhi ya fedha ya kigeni Nchini. Sekta ya madini imeipiku sekta ya utalii.
-> Migogoro baina ya Serikali na Barrick itatatuliwa kwa kutumia kanuni zilizowekwa katika mkataba bila kulazimishwa kutumia taratibu na sheria za nje. Hivyo hata kesi zilizoanzishwa katika Mahakama za usuluhishi Nchini Uingereza zipo mbioni kuondolewa ili kukidhi masharti ya mkataba.
-> Uchimbaji wa madini lazima utumie wataalamu wazawa na kutumia huduma za ndani ya Nchi ili kutoa kipaumbele kwa wafanyabiashara Watanzania.
-> Mamlaka yenye jukumu la kutoa taarifa kuhusu sekta ya Madini ni Kamisheni ya Madini na siyo mzushi THABITI JACOB kutoka Denmark. Maswali yaliyoulizwa na BBC yalipaswa kuelekezwa kwa Kamisheni hiyo. Kitendo kilichofanywa na BBC kililenga kupotosha na kuchafua taswira ya Nchi. Bado BBC kama ina nia njema inaweza kupata uthibitisho kutoka Kamisheni ya Madini Nchini Tanzania.
Maoni
Chapisha Maoni