MIPANGO ILIYOANDALIWA KUIINGIZA TANZANIA KATIKA MACHAFUKO KIPINDI CHA UCHAGUZI MKUU



Mipango hiyo imewekwa bayana kupitia mahojiano yaliyofanyika kati ya Mtangazaji wa Swahili villa online Tv Dk. Patrick Nhingula na Wakili wa Tundu Lissu Bw. Robart Amsterdam akiwa Instarbul Nchini Uturuki. 

Katika mahojiano hayo imeelezwa mipango hiyo bila chembe ya aibu ikizingatiwa kuwa Tanzania ni Nchi huru inayofuata utawala wa kisheria na misingi ya kidemokrasia kama zinavyofanya Nchi nyingine Duniani. 

Mipango hiyo imethibitiswa kwa kauli nne alizozitoa wakili Robert Amsterdam ambazo ni:-

1. UCHOCHEZI WA FUJO NA MACHAFUKO KWA VYAMA VYA UPINZANI

Amsterdam amekiri na kuthibitisha kwa kinywa chake kuwa yeye na timu yake wameamua kuwa wachochezi wa vitendo vya fujo ili kuharibu amani iliyopo Tanzania kwa kushirikiana na baadhi ya vyama vya upinzani Nchini.

Bw.Robart Amsterdam ametoa madai ambayo siyo ya kweli kudai kuwa kwa muda mrefu viongozi wa vyama vya upinzani Nchini Tanzania wamefungwa midomo. Hivyo, ameeleza kuwa atahakikisha anaunga mkono vyama vya upinzani katika kufanya fujo na kuleta machafuko.

2. MAANDAMANO

Robert Amsterdam anaratibu mpango wa kuhamasisha maandamano ili kuchochea fujo na machafuko Nchini Tanzania ili iwe rahisi kwa yeye kupenyeza vikundi vya kigaidi vitakavyokuwa upande wa kundi la vyama vya upinzani kuendesha mapigano yatakayo sababisha mauaji kwa wananchi wasio na hatia na kisha lawama zitaelekezwa kwa Serikali  iliyopo madarakani chini ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Lengo ni kuwa pindi mauaji yatakapotokea kuitishwe wito wa Upatanisho, Jumuiya za kimataifa ziite pande zote (vyama vya upinzani na CCM)  kuwapatanisha na kuwataka kuunda Serikali Mseto ambayo hata katiba ya Nchi yetu hairuhusu suala hilo. Kupitia mpango huo azima yao itakuwa imetimia ya kuwatumia viongozi wa vyama vya upinzani katika kunyonya rasilimali za Nchi yetu.

3. USALAMA WA TUNDU LISSU

Robert Amsterdam anajua kuwa mteja wake Tundu Lissu hawezi kushinda nafasi ya Urais katika Uchaguzi Mkuu, suala ambalo litasababisha ashindwe kufanikisha malengo yake. 

Kufuatia kauli aliyoitoa Robert Amsterdam kuwa “Tundu Lissu hawezi kuwa salama kama Serikali haitaondoka madarakani” inaonesha kuwa kauli  hiyo itatumika kama ajenda ya kuhamasisha wananchi kuingia kwenye machafuko kwa kigezo cha kudai usalama wa Lissu. 

Mpango huu umekuja ilihali Dunia nzima inashuhudia namna na jinsi Tundu Lissu anavyoendelea na shughuli zake za kisiasa katika hali ya usalama na amani tangu amerejee Nchini licha ya kuendelea kufanya mambo kinyume na sheria za Tanzania.

4. VIKOSI VYA JESHI LA POLISI ZANZIBAR

Juzi kwa makusudi makubwa Robart Asterdam aliweka kipande cha video kwenye akaunti yake ya twitter kuonesha magari yaliyoonekana ni ya Jeshi la Polisi Zanzibar kuwa ni maadalizi ya Seriakali kuhujumu Uchaguzi Mkuu Zanzibar, huku kukiwa hakuna taarifa yoyote ya ufafanuzi wa video hiyo kama ambavyo inatumiwa  kulichafua Tanzania. 

Kutoka na vitendo na kauli za Tundu lissu za vitisho vinadhihirisha kuwa kuna mipango ya machafuko inaratibiwa Nchini.

Watanzania tuendelee kumuomba Mungu na kuombea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28, 2020 ufanyike katika hali ya utulivu na amani, atuepushe dhidi ya maadui hawa waliojipanga kuharibu na kuvuruga amani ya Nchi yetu tuliyoitunza kwa muda mrefu tangu tupate uhuru.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Manufaa ya Ushirikiano wa Tanzania na Kenya

BE AWARE, Robert Amsterdam is a Canadian Set to Plant Violence in African Countries.

LICHA YA AHADI KUWA WANGESHIRIKIANA, LISSU NA MEMBE KILA MMOJA ANAGOMBEA “KIVYAKE.”