Manufaa ya Ushirikiano wa Tanzania na Kenya

 

Tanzania na Kenya zimekubaliana kushirikiana kuondoa vikwazo vya biashara na kufungua milango Zaidi ya kuwekeza na kuinua uchumi baina ya nchi zote mbili.

Makubaliano hayo yamefikiwa kufuatia Ziara ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan nchini Kenya ikiwa ni kuitikia mwaliko aliopewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyata.


Ziara hiyo imekuwa na mafanikio makubwa kwa nchi zote Mbili kwani kuanzia Tarehe 05/05/2021 vikwazo vya Wafanyabiara wa Tanzania kuingiza mahindi nchini Kenya vimeondolewa.

Pamoja na mafanikio hayo mambo mengine ya manufaa ni:-

Kujenga na kuendeleza utamaduni wa kukutana mara kwa mara, hii itasaidia kutatua changamoto ndogondogo zinazojitokeza.

Kushirikiana kwenye sekta ya utalii, kwamba badala ya kunyanganyana watalii busara itatumika kuwashawishi watalii kuongeza siku za kutembelea Kenya na Tanzania.

Vyombo vya ulinzi kushirikiana kulinda maeneo yote ili kusaidia kuwepo kwa utulivu na kutoa fursa ya shughuli za kibiashara na uwekezaji kushamiri.

Ujenzi wa miundo mbinu ya pamoja kusaidia kuimarisha mashirikiano ya kibiashara baina ya nchi zote mbili baadhi ya barabara zitakazojengwa ni Ramu Mombasa – Tanga – Bagamoyo hadi Dar es salaam yenye urefu wa Kilomita 454 ambayo itajengwa chini ya programu ya Afrika Mashariki, mradi mwingine ni Barabara ya Arusha- Holili – Taveta  yenye urefu wa Kilomita 260.

Kukamilisha Mifumo ya kutoa huduma katika vituo vya pamoja vya mpakani ambavyo ni horohoro, lungaluga na sirari  ili vitoe huduma kama ilivyo mpaka wa Namanga na Holili.

Tanzania kuuza umeme Kenya kwani miundombinu ya kusafirisha umeme mkubwa  kV 400 inajengwa kutoka Singida hadi Namanga.

Tanzania kuanza kuuza nishati ya gesi Kenya kutokana na makubaliano ya kuanza kutekeleza mradi wa ujenzi wa bomba la gesi kutoka Dar es salaam hadi Mombasa. 

Watanzania kwenda kufanya uwekezaji nchini Kenya bila vibali.

Kushirikiana katika kukabiliana na virusi vya  Corona.

Mawaziri wa pande zote mbili kutatua changamoto za wafanyabiashara wa pande zote kwa wakati.

Hivi vyote ni vichocheo vya kukuza uchumi wa Tanzania na Kenya, utekelezaji mahususi wa makubaliano hayo utasaidia kuongeza uwezo wa kuzalisha bidhaa zinazoingizwa katika mataifa yote mawili pamoja na kuzalisha ajira kwa raia wake. 

Vilevile mapato ya mataifa hayo yatapanda mfano Tanzania kama sasa ilikuwa inapata mapato ya kiasi cha dolla bilioni 1.7 kutokana na  Wakenya kuwekeza nchini Tanzania, hivyo Makubaliano haya yatakuza mapato mara tatu ya awali.

Huu ni wito kwa raia wa Tanzania na Kenya kutumia fursa ya makubaliano hayo kufanya biashara katika nchi hizo.

Umoja ni Nguvu

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

BE AWARE, Robert Amsterdam is a Canadian Set to Plant Violence in African Countries.

Ujumbe wa Wakili Msomi kwa Wanaharakati wa Kenya

DAVID KAFULILA APANGUA HOJA 7 ZA TUNDU LISSU KWA TAKWIMU